Our Feeds

Saturday, 13 February 2016

Unknown

ORODHA YA VILABU VINAVYO ONGOZA KWA UDHAMINI




KLABU

Real Madrid yatia saini mkataba wa donge nono na Adidas kwa ajili ya udhamini wa jezi

Gazeti la Marca nchini Uhispania limechapisha orodha ya vilabu vya soka barani Ulaya vinavyoongoza kwa udhamini wa jezi.

Real Madrid imeonekana kuongoza orodha hiyo baada ya kupewa mkataba wa donge nono na wadhamini wao Adidas.

Kulingana na taarifa hizo, Real Madrid inatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka 10 na Adidas utakaowaingizia mapato ya fedha Euro milioni 140.

Endapo mkataba huo utatiwa saini, Real Madrid itakuwa kilabu yenye udhamini wa fedha nyingi zaidi duniani.

Ifuatayo ni orodha kamili ya vilabu 10 vilivyokuwa na mikataba ya fedha nyingi zaidi na wadhamini wao wa jezi;

1. Real Madrid – Euro milioni 140 (Adidas 2016-2026)

2. Manchester United – Euro milioni 98 (Adidas 2014-2025)

3. Bayern Munich – Euro milioni 80 (Adidas 2015-2030)

4. Chelsea – Euro milioni 39 (Adidas 2013-2023)

5. Arsenal – Euro milioni 39 (Puma 2013-2018)

6. Liverpool – Euro milioni 32 (Warrior 2012-2018)

7. Barcelona – Euro milioni 32 (Nike 2008-2018)

8. Juventus – Euro milioni 26 (Adidas 2013-2021)

9. Milan – Euro milioni 23 (Adidas 2013-2023)

10. Paris Sanit Germain – Euro milioni 23 (Nike 2014-2015)

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »