Star
wa Bongo Movies Vicent Kigosi ‘Ray’ (aliyevaa kofia nyeusi) akifatilia
kwa makini mchezo wa Yanga dhidi ya Simba. Ray ni shabiki mkubwa wa
Yanga SC
Mchezo wa Simba vs Yanga hushuhudiwa na mashabiki lukuki Tanzania,
Afrika Mashariki na Kati lakini katika mchezo wa leo (Jumamosi February
20, 2016) kuna watu wenye majina makubwa bongo walikuwepo kushuhudia
mchezo huo.
Wapo ambao waliweka mapenzi yao wazi kwa kuvaa jezi za timu
wanazozishabikia lakini wapo pia ambao hawakutaka kuonekana wako upande
upi kati ya timu hizo mbili.
Angalia picha za baadhi ya ma-star hao walioibuka uwanja wa taifa kujionea wenyewe live game ya Dar es Salaam Derby.
Mawaziri wa serikali ya awamu ya tano Mwigulu Nchemba (katikati) na Nape
Nnauye (kulia) walikuwepo uwanja wa taifa kuangalia mtanange wa Yanga
vs Simba
Mwenyekiti
wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe (aliyevaa kofia)
akiwa amesimama kusuhudia namna ambavyo Simba ikikwama mbele ya YangaBaada ya ushindi ni sherehe, Ray akifungua kinywaji kufurahia ushindi wa Yanga baada ya kuifunga Simba kwa bao 2-0Kamanda
wa polisi mstaafu wa jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto juu)
alikuwepo kushuhudia pambano la watani wa jadi Yanga vs SimbaWaziri wa zamani Profesor Juma KapuyaSuperstar
mwingine wa Bongo Movies JB akiwa nje ya uwanja muda mfupi kabla ya
pambano la Yanga vs Simba halijaanza, JB ni mnazi mkubwa wa mnyama wa
Msimbazi