TANZIA: KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA ZANZIBAR AFARIKI DUNIA
Na Martha Magawa,
Zanzibar
Aliyekuwa katibu mkuu wa ZFA taifa Pemba ABDALLAH SULEIMAN SHARIF amefariki mchana huu mara baadaya kuanguka ghafla wakati alipokuwa akiendelea na zoezi la usimamizi wa ujenzi wa nyumba yake iliyopo mtambwe wilaya ya wete mkoa wa kaskazini Pemba.
Mara baadaya kuanguka alikimbizwa hospitali kuu ya Wete na baadaya ya vipimo alionekana tayari amekwisha fariki.