Our Feeds

Sunday, 21 February 2016

Unknown

Tathmini ya mchezo wa jana kati ya Simba na Yanga

JACOB GAMALY

JANA katika dimba kuu la taifa ,ule ushindani na tambao za nani atakuwa mbabe wa mwenzake kwa msimu huu wa ligi kuu baina ya miamba ya soka nchini Simba na Yanga ulitamatishwa mara baada ya mabingwa wa tetezi wa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga Sc kuibanjua Simba goli 2-0.

Matokeo haya ambayo yamepokelewa kwa mshtuko mkubwa miongoni mwa wapenzi ya Simba ambao waliamini kuwa wangeweza kuibuka na ushindi kutokana na kasi ya kikosi chao katika baadhi ya mechi za hivi karibuni,lakini si tu hivyo bali pia walitumai kuwa hata kama wasingeweza kuibuka na ushindi basi huenda wangetoka sare na watani zao hao.

Kumbuka pia hali kama hii ilitokea katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu huu ambapo mechi baina ya miamba hiyo ilitamatika kwa Yanga kuichabanga Simba goli 2-0.

Nini kiliimaliza Simba?hili ni swali ambalo mashabiki wengi wa soka bila shaka watakuwa wanajiuliza hasa ukizingatia kuwa timu hiyo toka ilipoanza kunolewa na mwalimu Mayanja imekuwa na moto wa kuotea mbali katika baadhi ya mechi zake,sawli hilo linajibiwa na hoja hizi nne kubwa..

1.Kadi nyekundu ya haraka.

Kwa kawaida timu huwa na kushuka kwa morali pale inapotokea mmoja katika ya watu wanaotegemewa kuwa hayupo katika eneo analostahiki kuwemo,pamoja na kwamba huweza kustahimili vishindo kutoka kwa timu pinzani lakini hali hiyo hutegemeana na ni muda gani pengo la mtu husika hujitokeza,katika dakika ya 25 Simba wanajaribu kuzuia pengo la moja kati ya wachezaji muhimu katika mchezo wa jana (Abdi Banda) na kujikuta wachezaji wengi hususani eneo la kiungo cha chini wakijaribu kulifunika pengo la mchezaji huyo na wakati huo huo wakitimiza wajibu wao katika maeneo yao wanayostahili kucheza kitu ambacho ni kigumu katika hali ya kawaida.

Kutoka kwa Banda ambapo kuliokana na kumfanyia faulo mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma kulipunguza pia morali ya kupamba ya timu ya Simba na kujikuta wakicheza kwa hofu muda wote wa mchezo kuhofia kuwa huenda angeweza kutolewa mchezaji mwingine.

2.Kutokuwa na mawasiliano mazuri baina ya beki na golikipa.

Katia ya vitu ambavyo huenda mshambualijai wa Yanga Donald Ngoma huwa hafanyi makosa,ni pamoja na jinsi ya kujua kucheza na akili za mabeki wa timu pinzani lakini pia kuwafuatilia ni nini wanafanya na ni kwa wakati gani wanafanya katika kumchunga yeye,anatumia udhaifu uliochangiwa na kushuka kwa morali kwa wachezaji wa Simba mara baada ya kuwa pungufu ambapo pia ulipelekea kila mchezaji kucheza kivyake ili kusudi kuepusha lawama hali inayopelekea kukosa mawasiliano baina ya wachezaji,mathalani goli ambalo analifunga Ngoma lilitokana na kutokuwepo kwa mawasiliano baina ya golikipa na beki wake(Ramadhani Kessy na Vicent Agbani ),maana katika hali ya kawaida tu beki anapotaka kurudisha mpira kwa golikpia wake sharti la kwanza ni lazima amwite kwa sauti ili kusudi golikipa awe shapu katika kujihami na kuchukau hatua.

3.Kuanza pamoja kati ya Amis Kiiza na Ibrahimu Ajib.

Ni vigumu kuelewa hili kama utakuwa na mhemko wa kishabiki nadni yake,ila moja kati ya sababu nilizoona ambazo kwa namna moja au nyingine ziliimaliza Simba ni pamoja na kuwaanzisha waxgezaji hawa pamoja,si kwamba ni wabaya ,la!hasha bali kila mmoja katia ya hawa ana uzuri wake kulingana na namna unavyomchezesha,mathalani jana kati ya vitu ambavyo viliujaza moyo wa Kiiza ni kuona anatimiza adhama yake ya kuifunga Yanga(alikuwa na uchu uliopitiliza ambao hukumsaidi katika kutimiza lengo) na hii ni kutokana na kuwa katika mechi iliyopita baina ya timu hizi aliwaaminisha mashabiki wa Simba kuwa lazima awe 'mtumbaji' kila anapokuta na timu yake hiyo ya zamani matokeo yake kwenye mechi ya kwanza akashindwa na hata katika mechi hii pia aliinga dimbani akijua ni lazima aifunge Yanga,sasa hapa ndio tungejua umakini wa Mwalimu Mayanja katika kucheza na akili na saikolojia ya wachezaji wake,ingekuwa busara sana kama Kiiza angeanzia Benchi ili atulize munkari yake lakini pia angekuwa mtu sahihi wa kwenda kubadili matokeo katika kipindi cha pili,badala yake angemuanzisha Ibrahim Ajib na Danny Lyanga ambaye anaonekana kuwa mahiri kadri siku zinavyoenda.

4.Mabadiliko ya kipindi cha pili.

Ni vigumu kupuuza umuhimu wa mtu kama Awadhi Juma katika mechi kama hizi,pamoja na kwamba Lufungo nimmoja katika ya wachezaji wanaokuja kasi nchini huku akiwa na soka maridhawa lenye tija dimbani lakini suala la uzoefu na tija dimbani lilipaswa liwe kigezo cha kuongoza busara za mwaliu Mayanja katika kufanya mabadiliko ya kumtoa Mwinyi Kazimoto na kumwingiza Lufungo ambaye hii ni mechi yake ya kwanza kubwa,tofauti na mtu kama Awadhi JUma au Mussa Mgosi ambao wote wawili wanaudhoefu wa kutosha na mechi za namna hii.



Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »