Our Feeds

Tuesday, 23 February 2016

Unknown

TFF ESTER CHABURUMA NI HAZINA.

Na Albogast
"Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na Mwisho" Na kama tungekuwa na Mipango,Uwekezaji, na Utekelezaji basi jina la CHABURUMA lingeishi miaka yote kutokana na uhalisia kwamba ESTER aliwaaminisha wanawake wengi kuwa Soka si la wanaume peke yao hata hapa Tanzania tunaweza kuwa na Timu ya wanawake na 2002 rasmi ikaanza Twiga Stars chini yake kama Captain.

November 07 mwaka jana ndio siku ambayo nyota huyu aliamua kuachana na soka ili kutoa nafasi kwa wengine,
Hii ilikua ni katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Tanzania na Malawi lakini sishangai kuona ni miezi tu na siku kadhaa jina hili linapotea sijui ni kwasababu mwaka 2015 ulikuwa na mambo mengi kama uchaguzi au ni kwasababu hatujali na kuthamini michango na kujitolea kwa watu kuwakilisha taifa lao.
Inasikitisha kuona TFF hawahangaiki hata kumusomesha Chaburuma ili awe na taaluma ya ukocha ili kumwandaa kuja kutumika kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars kama ambavyo nchi zingine zinafanya na hatimaye soka lao linakua siku hadi siku lakini kwetu hapa mambo ni tofauti hata ile heshima tu aliyositahili Ester kama shujaa wa taifa hajapewa.
Kumbukumbu zangu zinaniaminisha kuwa Twiga Stars chini ya Ester imefanya vizuri kimataifa kuliko Taifa Stars kwa maana hiyo kama ni ushujaa wanastahili kupewa Twiga stars amba walikuwa chini ya Capteni Ester Chaburuma.
Bahati nzuri Ester amecheza kipindi kimoja na nguri wa soka la wanawake na mchezaji bora mara tano Marta Vieira da Silva mwanamke wa kibrazil ambaye aliwafanya AC MILAN kutamani kumsajili ili achezee timu yao lakini sheria za soka la wanaume ziliwabana kutokana na kutoruhusu mwanamke kucheza timu ya wanaume hivyo naamini Ester amejifunza mengi kutoka kwa huyu dada na anao uwezo wa kuinua soka la wanawake Tanzania kama atapewa nafasi ya kupata mafunzo.
Kwasasa Marta ni mshauri wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake ya brazil na sitoshangaa baada ya muda kumuona akiwa kocha mkuu wa timu hiyo lakini kwa Chaburuma ni tofauti ikiwa tayari ameshaanza kusahaurika na kupotea kwenye ramani ya soka la wanawake Tanzania japo alistahili kustaafu kwa heshima kama si kwenda Bungeni kama tulivyozoea ukifanya vizuri unakwenda pale mjengoni Dodoma basi hata angetembezwa kwenye gari la wazi kutoka TFF hadi uwanja wa taifa ambako ilifanyika mechi ya mwisho siku anastaafu, naamini hii ingesaidia kuwataminisha wadogo zake kufikia mafanikio yake na hatimaye kupata heshima kama hiyo lakini mambo haykuwa hivyo.
Kuna msemo unaosema “tunajifunza kutoka kwa waliofanikwa” maana na dhamira ya msemo huu haiwezi kueleweka kama waliofanikiwa hawapewi heshima wanayostahili na kuthaminiwa kwa mchango wao ili wengine nao watamani mafanikio hayo.
TFF hii ni aibu tafadhali iondoeni kwa kumuenzi Ester, wakati pale Mbagala panajengwa sanamu ya Samatta natamani kuona pale Karume panajengwa sanamu ya Ester.


Asante ESTER kwa kutupeleka kwenye fainali za michuano ya Afrika mwaka 2010  kitu ambacho kwa Taifa Stars imekuwa ndoto isiyo na Mwisho na Asante tena kwa kutupeleka kwenye fainali za ALL AFRIKA GAME 2011.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »