Na Albogast Benjamin
Historia zipo ili siku moja watu wazima waweze kusimulia kizazi kipya ambacho huenda hakikupata kushuhudia yale ya kihistoria yaliyopata kutokea miaka mingi nyuma, Unaikumbuka April 5 mwaka 2006? Je unatambua kama mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali ya Uefa Barcelona dhidi ya Atletico De Madrid umechezwa tarehe moja na robo fainali ya mwaka 2006?
HII NDIO HISTORIA NINAYOMAANISHA
April 5 Benfica alikuwa ugenini kwa Bayern pale Allianz Arena jijini Munich lakini siku hiyo hiyo mwaka 2006 yaani miaka 10 iliyopita Benfica alikuwa ugenini kwa Barcelona kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ambapo mchezo huo uliisha bila kufungana kabla ya Barcelona kushinda mabao mawili kwa sifuri wakiwa nyumbani na kutinga nusu fainali hadi fainali ambako walitwaa ubingwa dhidi ya Arsenal.
![]() |
Picha aliyoweka Ronaldinho kwenye ukurasa wake wa Instagram kama kumbukumbu ya mchezo huo wa April 5 |
WACHEZAJI GANI WALIKUWA VINARA WAKATA HUO?
Hakika hii ni kumbukumbu kubwa sana kwa mchezo wa soka maana lazima uwakumbuke watu kama Ronaldinho,Deco na Eto'o wakati Arsenal unawakumbuka Thiery Henry, Vierra na Sol Campbell.
MATOKEO YA MECHI ZA APRIL 2016.
Usiku wa Ulaya uliendelea usiku wa April 5 ambapo mechi mbili za robo fainali zilipigwa Bayern wakiwa nyumbani walishinda 1 - 0 dhidi ya Benifica bao la Artulo Vidal wakati Barcelona wakiwa nyumbani walishinda 2 - 1 dhidi ya Atletico Madrid mabao ya Barca yakifungwa na Luis Suarez Dk63,74 wakati la Atletco lilifungwa na Torres Dk25 kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu Dk36.