Our Feeds

Tuesday, 12 April 2016

Unknown

NIGERIA HATARINI KUUA SOKA LA NCHI YAO KWA KIFUNGO

Na Albogast Benjamin
Mei18,2015 ndo siku iliyotolewa hukumu na mahakama ya michezo KAS, iliyotoa kibali cha rais wa shirikisho la soka Nigeria NFF Amaju Pinnick kuendelea na madaraka lakini kwasasa mambo yamemwendea kombo.
Rais wa NFF Amaju Pinnick aliondolewa madarakani Alhamisi iliyopita baada ya mahakama moja kuamua kuwa kiongozi wa sasa Pinnick alishindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka wa 2014.nMahakama ilisema kuwa Chris Giwa ndiye anayefaa kuwa rais wa shirikisho la soka la Nigeria NFF. 
FIFA imeonya kuwa Nigeria imo katika hatari ya kupigwa marufuku endapo itatekeleza uamuzi wa mahakama. Katika taarifa iliyotumwa kwa serikali ya Nigeria Jumatatu tarehe 11 Aprili kaimu katibu wa FIFA Markus Kattner, anasema uamuzi huo wa mahakama unatafsiriwa kama kuingiliwa kati kwa maswala ya kandana.
''Bila shaka uamuzi wa mahakama unafasiriwa kuwa ni kuhitilafu uendeshaji wa shirikisho na hiyo bila shaka inakiuka kanuni za FIFA ambazo haziruhusu maswala ya kandanda kuamuliwa mahakamani.'' alisema bw Kattner

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »