Viongozi wa Premier League Leicester mpaka sasa wamepoteza mechi mbili katika msimu huu, mara moja kati ya hizo ilikuwa ni kipigo kizito cha 5-2 kutoka kwa Arsenal katika dimba lao la King Power mnamo September 2015. Wikiendi timu hizi mbili zinakutana tena, je Gunners wataweza kuutafuna mfupa mgumu uliowashinda wengi msimu huu?

Staili ya ushambuliaji ya Arsenal iliweza kuutumia udhaifu wa Leicester ambao timu nyingi wameshindwa kuutumia. Wakati huo, Claudio Ranieri alikuwa bado hajafanikiwa kupata clean sheet hata moja lakini tatizo hilo la ulinzi limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa tangu wakati huo. Kwa kifupi Leicester wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 3 katika mechi 8 zilizopita – idadi ambayo Alexis Sanchez aliifanikisha ndani ya dakika 48 tu za mchezo mnamo September.



Hakuna ubishi kwamba hawa wawili ni moja ya nguzo muhimu ya mafanikio ya Leicester msimu huu lakini katika mechi iliyopita dhidi ya Gunners walikuwa na siku mbaya. Wawili hao walizimwa, Mahrez alitulizwa vizuri, alipoteza mipira mara 26, zaidi ya mchezaji yoyote yule kwenye mechi hiyo. Vardy alifunga mara mbili lakini magoli yake hayakusaidia lolote mwisho wa siku – japo alimsumbua sana Marteseker, na hilo linaweza kumfanya Wenger ampange Gabriel wikiendi hii.
Staili ya uchezaji!
Tatizo ambalo linaweza kuwapa presha mashabiki wa Leicester sio wachezaji bali staili ya uchezaji ya Arsenal na mbinu atakazoingia nazo Ranieri.
Tatizo ambalo linaweza kuwapa presha mashabiki wa Leicester sio wachezaji bali staili ya uchezaji ya Arsenal na mbinu atakazoingia nazo Ranieri.

Leicester wana rekodi nzuri ya kupata pointi nyingi ugenini kuliko timu yoyote katika EPL msimu huu, na wamebadilika kiuchezaji tangu walipokutana na Gunners mara ya mwisho – hata hivyo Ranieri anatarajia kuwaanzisha wachezaji 9 kati ya walioanza mechi iliyopita – je watafanikiwa kulipa kisasi, tukutane Jumapili usiku kwa ajili ya matokeo ya mchezo huu muhimu kwenye mbio za ubingwa wa England.