Our Feeds

Saturday, 13 February 2016

Unknown

VPL: NI SIMBA SC AU AZAM FC KUISHUSHA YANGA KILELENI?


Beki wa Simba Mohamed Hussein 'Tshabalala' akimtoka beki wa Azam FC Shomari Kapombe

Beki wa Simba Mohamed Hussein 'Tshabalala' akimtoka beki wa Azam FC Shomari Kapombe








Beki wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa Azam FC Shomari Kapombe

LIGI kuu ya kandanda Tanzania Bara, VPL itaendelea tena wikendi hii katika mzunguko wake wa 19. Ni timu mbili tu hazitakuwa na mechi za VPL kati ya timu zote 16 kbtika siku za Jumamosi na Jumapili.
Vinara Yanga SC watakuwa katika harakati zao za mwanzo katika kampeni yao ya kucheza nane bora ya mabingwa wa Afrika hivyo mchezo wao na Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umesogezwa mbele katika tarehe itakayotangazwa na bodi ya ligi.
Kutokucheza kwa mabingwa hao watetezi kunaweza kutoa nafasi kwa timu za Simba SC na Azam FC kukaa juu yao katika msimamo kama tu watafanikiwa kupata ushindi katika michezo yao ya kesho Jumamosi na siku ya Jumapili.
STAND UNITED v SIMBA SC
Mechi hii ni muhimu kwa kila timu lakini itakuwa na manufaa zaidi kwa Simba kwa maana kama watapata ushindi wataenda kileleni kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu. Japo inaweza kuwa kwa masaa 24 tu lakini ni jambo zuri kwa ‘Wekundu wa Msimbazi’ kupata ushindi.
Stand ni timu ngumu kwa Simba na inaundwa na wachezaji wengi wazoefu katika ligi inaweza kufanya lolote na usishangae wakaifunga tena Simba kama walivyofanya msimu uliopita katika uwanja wa Kambarage.
Mechi nyingine itakuwa ni ile ya MbeyaCity FC ambayo itakamkaribisha kwa mara ya kwanza katika ligi kuu kocha raia wa Malawi, Kinnah Phiri. City hawana matokeo mazuri msimu huu watacheza na ‘Wabishi’ Toto Africans ya Mwanza.
Mwadui FC baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya ugenini dhidi ya African Sports katika uwanja wa Mkwakwani kisha mbele ya Azam FC katika uwanja wa Chamanzi, Dar es Salaam itarudi nyumbani, Mwadui Complex, Shinyanga kucheza na timu isiyotabirika-Tanzania Prisons ya Mbeya.
Hii itakuwa vita ya timu zilizo katika nafasi ya 6 na 7, na wenyeji watapaswa kumchunga sana mshambulizi, Jeremiah Juma na patna wake Mohamed Mkopi ambao kwa pamoja wamefunga jumla ya magoli 16.
Mwadui FC chini ya kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ imeonekana kupwaya katika safu ya mashambulizi tangu kuondoka kwa mshambuliaji Paul Nonga aliyejiunga na Yanga katika usajili mdogo mwezi Disemba, 2015.
Jerson Tegete amekwishafunga magoli matano msimu huu na mchezaji huyo wa zamani wa Yanga anapaswa kuwa mtulivu zaidi ili kufunga nafasi nyingi za magoli. Kushindwa kupata goli dhidi ya Sports na Azam si sababu ya kuanguka tena mbele ya Tanzania Prisons na kushindwa kufunga walau goli moja kwa kikosi cha Julio itakuwa ni sawa na kukubali kipigo cha tatu mfululizo.
Prisons ilifunga magoli mawili walipokaribia kuifunga Yanga na wakashindwa kufunga katika ‘Mbeya derby’ dhidi ya Mbeya City katika michezo miwili iliyopita lakini wanajivunia mastraika wao wenye uwezo mkubwa wa kufunga. Itakuwa ni bonge la mechi kati ya vijana wa Salum Mayanga na wale wa Julio.
Mechi ya Coastal Union na Azam FC pia itafuatiliwa sana kwa kuwa Azam wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama sawa na Simba (42.) Coastal ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuwafunga mabingwa watetezi Yanga msimu huu.
Ushindi wa 2-0 dhidi ya Yanga haukutarajiwa, Azam wanakwenda Tanga wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu
Sat 13/02/16
Stand United vs Simba SC
JKT Mgambo vs African Sports
Mbeya City vs Toto Africans
Ndanda SC vs Maji Maji FC
Ruvu JKT vs Kagera Sugar
……………………………….
Sun 14/02/16
Mwadui FC vs Tanzania Prisons
Coastal Union vs Azam FC

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »