Na Albogast
Mipango,Uwekezaji na Utekelezaji vikifanyiwa kazi vyema hivi vitu vitatu matokeo yake lazima yashangaze wengi kama sio kufaidisha wengi.
Hivi vitu vitatu ndani ya Azam fc vinatimia ndio maana wanapopata mafanikio kimya kimya wengi wanahisi wanabahatisha japo ukweli ni kwamba bado wanasafari ndefu lakini hawawezi kufikisha miaka ya Simba na Yanga bila kufika zilipo TP Mazembe,Kaizer chiefs na zingine kama El merreik ya Sudan labda iwe imepotea kabisa kwenye ramani ya soka.
Napata jeuri ya kusema haya kutokana na ukweli kwamba Azam ipo chini ya kampuni tajiri tena inamilikiwa na tajiri mwenye uwezo mkubwa wa kuwekeza,maana yangu hapa Bhakhresa Group of Company hawawezi kukubali Azam iendeshwe kwa hasara mana wanajua inawagharmu kiasi gani ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji na makocha hivyo kwa namna moja lazima wafike walipokusudia ili kukaribisha wawekezaji zaidi watakaoweza kufanya biashara na Azam pindi itakapokuwa moja ya kilabu kubwa barani afrika kama tunavyoshuhudia makampuni makubwa yakiwekeza kwenye vilabu kama Madrid au Barcelona kwasababu wanakuwa na wigo mpana wa kutangaza biashara zao.
1. Mipango
Azam FC toka imepanda daraja imekuwa ikifanya vizuri kutokana na mipango iliyokuwa nayo na mikakati pia, Lengo la kwanza la timu hiyo ilikuwa ni kushiriki ligi kuu bara jambo ambalo viongozi walisimamia na likawezekana, Lengo la pili ilikuwa ni kushika nafasi itakayo wafanya wawakilishe taifa katika michuano ya CAF pia hilo liliwezekana kwani wameshika nafasi ya pili mara kadhaa na Lengo la tatu lilikuwa kubeba ubingwa wa bara na hatimaye pia wamefanikiwa kutwaa ndoo hiyo.
2. Uwekezaji
Timu ambazo zinaongozwa kwamfumo wa kampuni duniani kote huwa zinafanya vizuri kutokana na kampuni kuwa na mipango yake na malengo ambayo hujiwekea na hutoa muda ili kuyafikia tofauti na wanachama ambao wao huwa wanatamani mafanikio ya haraka kitu ambacho hakiwezekani maana mtoto huzaliwa, hukaa, hutambaa alafu baadaye ndio hukimbia. Kwenye hili Kampuni ilitambua kuwa haikuanza kama ilivyosasa na ndio mana na timu imekuwa hivyo wameweka Mipango wakapanda ligi kuu na baadae wakaja kwenye Uwekezaji na ndio maana wakajenga uwanja na kuwa na Academy ambayo baadaye watakuwa na uwezo wa kukuza vijana na kuuza hatimaye klabu kujiendesha na kuapnua uwanja kutokana na mapato yake yenyewe bila kutegemea kampuni mama tena.
3. Utekelezaji
Mipango na Uwekezaji lazima utekelezwe na watu makini wenye kujua nini wanafanya na hivyo tu bali taaluma zao ziendane na majukumu wanayokabidhiwa kuyatekeleza na hapo ndio mafanikio yanakuja kama unapendelewa kumbe umetumia vizuri maneno haya matatu Mipango,Uwekezaji na Utekelezaji.
Hapa ndipo vilabu vingi vinashindwa kusimamia vyema kutokana na kuweka watu wasio na uwezo ama taaluma juu ya mchezo wa soka,nimeona kitu cha tofauti kwa Azam fc kutokana na uongozi wa kampuni kukaa pembeni na kubaki wasimamizi wa mambo ya fedha tu lakini mambo yanayohusu ufundi na timu uwanjani wakiyaacha kwa wataalamu wa soka kama.
i. Stewart Hall. huyu ndiye Kocha mkuu wa Azam FC na tunafahamu uwezo wake ambao ulitambulika hadi na Sunderland walipokuja kuwekeza kwenye mradi wa kukuza vipaji ndio walimpa jukumu la kusimamia kituo hicho kilichopewa jina la rais mstaafu JAKAYA YOUTH PARK. Baada kuvunja mkataba wake miaka michache iliyopita walijikuta wakigundua mapungufu na kuamua kumrejesha kundini mtaalamu huyo wa ufundi.
ii. Jemedali Said. Huyu ni Meneja mkuu wa Azam FC, Huwezi kuzungumzia soka la bongo usimtaje Jemedali Said amewahi kuichezea Taifa stars anaishi kwa mpira, anazungumza mpira na anaweza kutoa ushauri wa kiufundi.
iii. Philipo Alando. Huyu ni meneja mkuu wa Azam academy. Huwezi kuizungumzia Toto Afrika ya Mwanza ukaacha kumzungumzia Alando, wengi mnamjua kwa kazi yake uwanjani pia ameichezea Taifa stars kwahiyo anajua mpira bila shaka anamchango mkubwa katika klabu ya Azam FC.
Ukijumlisha vitu vyote hivi unagundua kuwa Azam inapita changamoto tu na si kwamb