Na Albogast
1. AKILI YA MCHEZO
Kuna kitu mhimu ambacho kwasasa kinapatikana kwenye Barcelona ya Enrique tofauti na Barcelona ya Qurdiola, Usiku wa jana umedhihirisha hilo baada ya akili ndogo tu ya Mchezo ambayo ni ngumu kugundua na kudhibiti akili hii ni pale unapowaona Barcelona wakiwa wamepoa hawapigi tena zile pasi nyingi hasa mara baada ya kusoma mchezo wa mpinzani na wanapata mpira wakati ambao mpinzani wamemvuta na akavutika kuja kushambulia kisha akapoteza mpira na wao kupitia mtaalam wa soka Iniesta anapiga pasi ndefu kwa Suarez anampa Neymar na Hatimae Messi anakuwa amefika wanahitimisha Kitu kinaitwa Counter Attack na kupata bao. Awali hawakuwa na aina hii na mara zote walisubiri kupiga pasi hadi eneo la 6 ndo wafunge kitu ambacho kwa sasa ni tofauti.
2. ARSENAL KUAMUA KUSAKA GOLI
Dakika za mwanzo za mchezo Arsenal walimudu kucheza kwa kujihami huku wakishambulia kwa kushitukiza hali iliyofanya mchezo kuwa mgumu tofauti na watu walivyotegemea ambapo timu zote zilitengeneza nafasi lakini hakuna aliyefanikiwa kuzitumia vizuri,Kipindi cha pili Barcelona walizidisha kasi ya kushambulia kitu kilichowafanya Asernal waamke tena na kuanza kusaka goli ili kujiweka vyema Mechi ya marudiano, ndipo ilipowagharimu kwani Iniesta alipata muda mzuri wa kuwasoma wanavyokuja kisha akajua jinsi gani watapata mpira kisha kufikisha mbele kwa Neymar ambaye alionekana mara nyingi kukaa peke yake ama na beki mmoja hadi wawili kitu ambacho kwake si hofu anaweza kuwakimbiza kwa madoido yake huku akijua wazi Messi au Suarez wanakuja na pindi watakapofika aweze kuwalisha na kufanya kilichowaleta.
3. UJANJA WA MESSI AKIWA ENEO LA HATARI
Unapomzungumzia Messi unaona ni mtu mwenye akili nyingi sana za mchezo na katika mchezo huo ilimbidi arudi kumsaidia Dan Alves kupandisha mipira kutokana na zoezi hilo kuonekana limemshinda Alves ambaye mara nyingi alipokonywa na Sanchez,akili hii ya Messi iliwafanya walinzi wa Arsenal kumsahau na hapo ndipo utakumbuka wakati Neymar anakimbia na mpira Messi alikua peke yake wakati Neymar anakabwa na watu wawili na alipofanikiwa kuwatoka walinzi hao moja kwa moja akampasia Messi akiwa peke yake na kuweka kambani.
4. KUKOSA UMAKINI KWA FOWADI WA ARSENAL
Kipindi cha kwanza Arsenal walipata nafasi kadhaa lakini Giroud na Ramsey walishindwa kuzitumia kutokana na kukosa umakini kwa mfano pale golikipa wa Barcelona alikua ameanguka kwenye piga nikupige yashambulizi la Arsenal lakini Walimpasia mpira na kuudaka kitu ambacho upande wa pili tunaona Messi anapata nafasi anatulia anamtisha Peter Cech na kupiga sehemu iliyowazi akifunga bao la kwanza.
5. UWEPO WA "MSN"
Hii ni safu kali zaidi ya ushambuliaji kuwahi kutokea kwa mjibu wa takwimu za soka ikihusisha nguli wa soka kutoka America ya Kusini Messi,Suarez na Neymar.
Uwepo wa hawa watu uwanjani wanainyima fursa sehemu ya ulinzi kujitanua na hatimae unawaona kabisa Kipindi cha pili wananjaa na wanaonesha kutaka ushindi kwa mipango ya ushirikiano uwanjani na wanafanikiwa kuamua matokeo ya Mchezo hali iliyofanya ubao kusomeka 0 - 2 Dk 90.
RIPOTI YA TAKWIMU ZA MCHEZO.
#Dk10 za mwanzo Asernal walitawala mchezo wakijiamini zaidi na kufika langoni mwa Barcelona mara kadhaa.
#Dk15 possession 30 arsenal 70 barca
#Dk30 mpira umebalance timu zikishambuliana kwa zamu
#Dak45 Half Time bila Kufungana
#Dk48 Neymar anakosa goli
#Dk49 Walcot anaingia nafasi ya chamberlain aliyeonekana kupata maumivu baada yakugongana na Mascherano.
#Dk71 Messi anapata bao kwa assist nzuri ya Neymar baada ya kazi nzuri ya Iniesta na Suarez.
#Dk73 Welbeck anachukua nafasi ya Giroud
#Dk82 Flamini anachukua nafasi ya Coquelin
#Dk82 penalti Messi kaangushwa na Flamin na
Anafunga Goli la pili.
#Dk86 Ramsey anakosa goli baada ya kupata pasi nzuri ya Welbeck.
Wednesday, 24 February 2016
SABABU ZA BARCELONA KUTOKA NA USHINDI EMIRATES.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »