Na Albogast
Kocha wa Arsenal mzee Wenger anayonafasi ya kuifunga Barcelona klabu ambayo inatajwa kuwa bora zaidi duniani kwa sasa lakini kwa hesabu hizi Wenger anaweza kupata matokeo mbele ya Barcelona inayoongozwa na MSN yaani Messi,Suarez na Neymar.
1. HESABU YA KWANZA
Arsenal wanatakiwa kurelax na kubadili aina yao ya uchezaji ili isifanane na Barcelona kama ilivyozoeleka timu hizi zinacheza aina moja ya uchezaji japo Barcelona wanakuwa juu zaidi kutokana na kuwa na wachezaji wa daraja la dunia. Hapa Wachezaji wa Arsenal wanatakiwa kuvunja baadhi ya majukumu kwa mfano Ozil na Sanchez hawatakiwi kucheza kwenye half zone ya Barcelona bali wanatakiwa kucheza Karibu na mabeki wao ili pindi Barcelona wanapopoteza mpira waweza kuuupata kwa haraka na kupasiana wao wawili kisha kupiga pasi ndefu mbele kwa haraka wakiwapatia wachezaji kama Walcot na Chambarlain na Kwa kutumia uwezo wao wa kukimbia wanaweza kusababisha kupata bao mapema.
2. HESABU YA PILI
Mabeki na Viungo wa Arsenal wakubali kukaba kwa kwa kasi ili kuwapokonya mipira viungo wa Barcelona kama Iniesta na Messi ambae anatabia ya kurudi ndani na kunzisha mashambulizi hivyo inabidi wawadhibiti kabla hawajapiga mipira ya kuwafikia Neymar na Suarez.
3.HESABU YA TATU
Namba tatu inaenda kwa Ozil na Sanchez ambao wanatakiwa kuwa jukumu moja tu la kuhakikisha wanacheza kiungo cha Kushoto na Kulia ili Kublock mipira na kuwazuia Dan Alves na Jord Alba wasiweze kupanda na kusaidia mashambulizi kama ambavyo imezoeleka Barcelona huwatumia zaidi Fullback hawa kuanzisha mashambulizi na kama Ozil na Sanchez watafanikiwa katika hili wahakikishe wakipata mipira hiyo wanawalisha vyema Walcot na Giroud na kutokana na Kuwa Alves na Alba watakuwa wamepanda basi pasi hizo zinaweza kuzaa matunda maana walinzi wa kati wa Barcelona si wazuri sana wanapokuwa wenyewe bila usaidizi wa viungo wao.
4. HESABU NAMBA NNE
Kama Wenger anataka ushindi ni lazima awaanzishe Walcot na Chamberlain ili wasaidie kuwakimbiza kwa haraka zaidi mabeki wa Barcelona na ikiwezekana kabla viungo kama Busquet hawajarudi kukaba wawe tayari wamefika kwenye eneo la mwisho na ikiwezekana wapate bao.
5. HESABU YA TANO
Hesabu hii ni mhimu sana kama Wenger atakuwa amemfatilia vizuri mlinda mlango wa Barcelona anayetumika kwenye Michuano hii TerStergen atakuwa amegundua kuwa anatabia ya kutoka golini na kutorudi kwa wakati na hapo ndipo Ozil na Sanchez wanaweza kutumia udhaifu huo na kupiga mipira makini ya mbali ambayo inaweza kuzaa goli kama ambavyo ilikua kwenye Mechi ya Barcelona na As roma ambapo alifungwa bao la mbali sana lilioingia top3 ya mabao bora kwa mwaka jana.
HESABU YA MWISHO
Inaenda kwa Barcelona ambao kama ni Ufundi wa mpira wanao na wanaujua mpira hapa kazi ipo kwa Rakitic na Busquet kuhakikisha Sanchez na Ozil hawapati mipira na wakati huo Iniesta akimlisha mipira mingi Messi ambaye kwa pasi za mwisho kwenda kwa Suarez na Neymar hakuna mwenye Shaka na hilo. Hapa ndipo unaweza kuona Neymar anamsababishia mtu red kadi kutokana na style yake ya kukokota mipira.
Yote kwa Yote Dakika Tisini ndio msema kweli.
Wednesday, 24 February 2016
HESABU ZA MWISHO ARSENAL NA BARCA
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »