Mshindi wa Ballon d’Or Lionel Messi, ametangazwa kurudiwa namatatizo ya figo baada ya kushindwa kushiriki mazoezini.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na kilabu ya Barcelona, Messialibainishwa kurudiwa na matatizo ya figo yaliyowahi kumkumba mwezi Desemba mwaka jana.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Messi alifanyiwa ukaguzi wa afya na kusemekana kuwa ataweza kujiunga na kikosi cha Barcelona kwenye mechi itakayochezwa siku ya Jumatano.
Mnamo mwezi Desemba mwaka jana, Messi aliwahi kusumbuliwa na matatizo ya figo na kushindwa kuchezea Barcelona kwenye mechi dhidi Guangzhou Evergrande katika kombe la dunia la vilabu.