KWA MARA YA KWANZA MESSI ATWAA TUZO HII
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Laliga mwezi January ikiwa ni mara yake ya kwanza kubeba tuzo huyo.

Messi amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu ambao Barcelona hawajapoteza mechi 29 mfululizo.
Wakati Messi anapata tuzo hii ndio kwanza amerejea mazoezini na klabu yake baada ya kuwa nje kwa siku mbili akipata vipimo na matibabu ya figo ambayo imekuwa ikimsumbua mara kwa mara.