
MBWANA SAMATTA NDANI YA FIFA PLAYSTATION 16 GAME
DAR ES SALAAM
KWA mara ya kwanza mshambuliaji nyota wakimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta amejumuishwa katika kikosi cha FC GENK kwenye game ya playstation ya FIFA 16.
Kujumuishwa huku kwa mwanasoka bora huyo wa CAF kunaendeleza wimbi la mafanikio kwa mchezaji huyo ambaye alijiunga na timu ya FC GENK mwishoni mwa mwezi wa kwanza akitokea katika klabu ya TP Mazembe.
Mtembezi.com imepita katika maeneo maarufu ya watu wanapoenda kucheza game za FIFA Playstation na kukuta baadhi ya wapenzi wa mchezo huo wakifurahia kumchezesha mchezaji huyo akiwa katika kikosi cha timu ya FC GENK akiwa na jezi namba 77.
Hii inamaana kuwa hivi sasa huenda ligi ya Ubeligiji ikazidi kupata umaarufu sana hapa nchini kutokana na wapenzi wa game za FIFA Playstation watakuwa wakiichagua timu ya Samatta ili wafurahi kumchezesha mchezaji huyo wa zamani wa Simba Sc.
Hata hivyi inashauriwa kwa wale wote ambao wangependa kumchezesha Mbwana Samatta katika magame yao,ni vema wafanye ‘UP DATE’ kwanza ili waweze kuichagua timu ya FC GENK yenye uwepo wa Mbwana Samatta.
Hivi sasa Samatta yupo na timu yake akiwa katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo ujoa wa ligi ambapo watacheza na Lokeren Uwanja wa Daknamstadion katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Toka ajiunge na timu hiyo Mbwana Samatta bado hajafanikiwa kuifungia timu yake bao lolote lile,huku akiwa ameshuka dimbani mara mbili kuichezea klabu yake hiyo