Our Feeds

Saturday, 20 February 2016

Unknown

Nani ni nani Uwanja wa Taifa?




NA BARAKA KIZUGUTO, Dar
BAADA ya tambo za muda mrefu vigogo wa soka nchini timu za Simba na Yanga, leo jioni zitapepetana katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara, utakaochezwa Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zenye mashabiki wengi katika medani ya soka nchini zitachezeshwa na mwamuzi mwanamama Jonesia Rukyaa wa Kagera, ambaye atasaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo atakua Khalid Bitebo (Mwanza).
Taarifa iliyotumwa na Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto, ilisema kuwa milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru.
Alisema upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi, mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.
Shirikisho linawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »