Our Feeds

Tuesday, 16 February 2016

Unknown

Shabiki wa Arsenal ashangilia goli la Welbeck sana hadi sasa inahitaji operation.

Goli la dakika ya mwisho kwenye mechi ya Leicester City dhidi ya Arsenal iliwapa ushindi Arsenal na kuwaacha mashabiki wakiwa kwenye shamra shamra za kusherekea kupita kiasi.
coeg
Uzuri wa goli hilo ni kwamba limefungwa dakika za mwisho kabisa na aliyefunga ameekaa nje kwa muda wa miezi 10 na kurudi kufunga goli muhimu. Pia Arsenal walikua kwenye harakati za kupunguza gape kwenye mbio za ubingwa ukizingatia Leicester ndio wapo kwenye juu ya ligi.
Sasa shabiki mmoja anaitwa Scott Woods ameandika kwenye page yake ya Facebook kwamba goli lile la Welbeck limemfanya ashangililie hadi sasa hivi anahitaji kufanyiwa operation.
Kilichotokea ni kwamba huyu shabiki aliruka ghafla na kushangilia kwa kiasi kikubwa hadi ndani ya mwili wake organ moja ikahama kwenye position yake kidogo. Japokua hajaweka wazi ni organ gani mwilini mwake ambayo imekaa vibaya baada ya kujirusha sana akishangilia goli la Welbeck, bwana Scott amesema sasa hivi atafanyiwa operation ndogo kwa ajili ya kuweka vizuri hiyo organ.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »