NA MWANDISHI WETU, Pemba
NAHODHA wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema yuko vizuri kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi, utakaokwenda kuzikutanisha Simba na Yanga, Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.Cannavaro, aliyekuwa majeruhi ya muda mrefu tangu mwishoni mwa mwaka jana amesema yuko vizuri kucheza kwenye pambano hilo na hivi sasa ni jukumu la kocha wake Hans Van Pluijm, kumuamini ili afanye kazi yake uwanjani.Akizungumza na Simba Makini kisiwani hapa kwenye Uwanja wa Gombani, kwenye mazoezi ya leo asubuhi Cannavaro alisema yuko vizuri ndio maana yuko kambini na wachezaji wenzake hivi sasa.Alisema kaama angekuwa mgonjwaa muda huu asingfekuwaa kambini, hivyo kitendo chake cha kuambatana na timu kisiwani humo inaonyesha yuko tayari kwa mpambano.“Nimesharudi kikosini hivi sasa na niko tayari kwa ajili ya kazi ambazo nafahamu gfika kazi yangu hata hao washambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib na Hamis Kiiza ‘Diego’, wananijua vizuri.“Tusizungumze sana vilivyo nje ya mchezo. Yanga iko imara na mimi mwenyewe niko imara ndio maana unaniona na mimi niko hapa kwa ajili ya mchezo wetu huo unafuata ambao tunajua tunaenda kushinda” alisema Cannavaro.Cannavaro, aliwatoa wasiwasi mashabiki wa Yanga na kuwaambia wasitikishike na majina ya Ajib na Kiiza kutokana na viwango vyao vya hivi sasa na kusema wako tayari kuwazima.“Mimi naowaona kama wachezaji wengine ambao nimekuwa nikikutana nao uwanjani. Nimewahi kukutana nao mara nyingi lakini hakuna hata mwenye madhara ya kutudhuru, hivyo mashabiki wasubiri kuona tunavyoweza kuwazima washambuliaji hao na timu kuondoka na pointi tatu” alisema.
Friday, 19 February 2016
Cannavaro niko fiti asilimia 100 kuivaa Simba.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »