Na Amin Nyaungo
Mchezo wa mpira una maajabu yake kwa sasa, wachezaji nyota waliowahi kuzichezea timu zao ndio wanaapewa majukumu makubwa ya kuzifundisha. mfumo huu haswa umeanzia Hispania tumeona makocha mafanikio makubwa yamepatikana haswa imeamza kwa Pep Guadiola, Luis Enrique na Diego Simione.
Zinedine Zidane Zizou huyu fundi mwingine ambae naye amechukua madaraka pale Real Madrid na tangu aichukue timu hiyo haikufanya vibaya kwani amepoteza mchezo mmoja wa ligi na kushinda 11.
Lakini swali la wapenzi wa soka je atafanikiwa pale?
sio rahisi Real Madrid huwa wanataka maendeleo ya haraka anachotakiwa achague moja afanye vizuri aendelee au aharibu wamfukuze kama hawamjui hii ndio shukrani ya Real Madrid.
Zidane endapo ataifunga Barcelona na pia kuchukua ubingwa wa klabu bingwa barani humo ataweza kuwa salama, ilivyo Real Madrid ni kama 'figisu' za Simba na Yanga huwa wanaangalia zile mechi muhimu na mafanikio pekee hakuna kinacho angaliwa kingine ifuatayo ni rekodi ya Zinedine Zidane tangu apokee kijiti kutoka kwa Rafael Benitez
- Michezo 13
- Aliyo shinda 11
- Aliyo fungwa 1
- Aliyo toa sare 2
kwa rekodi hii inaonekana nzuri kuliko ya Benitez.
kwa rekodi hizi je, wakina Edi bin Lunyamila au Ally Mayai na Sekilojo chambua watapewa kazi Yanga? Simba tuliwahi kuona wakina Abdallah Kibadeni,J amhuri Kiwelu na Suleimani Matola wakipewa jukumu la kuinoa timu hiyo japo hawapewi muda mwingi.
- Michezo 13
- Aliyo shinda 11
- Aliyo fungwa 1
- Aliyo toa sare 2