Our Feeds

Friday, 1 April 2016

Unknown

SABABU ZA LIGI KUU ENGLAND KUPENDWA DUNIANI KOTE



Na Amin Nyaungo

Ligi kuu ya Uingereza imepiga hatua kubwa Duniani ambapo kila mmoja anavutiwa kuangalia mpira wa EPL, sasa unaijua sababu ya kupendwa? mambo mengi yamefanyika ilikuweza kushawishi watu kuipenda sio kazi rahisi.

PROMOTION(KUITANGAZA LIGI HIYO)
Kitendo  cha wapenzi wengi wa kandanda duniani kupenda ligi hiyo matokeo ya uwekezaji mkubwa ulio fanywa na chama cha soka cha nchi hiyo (FA) imetumia pesa nyingi kuitangaza ligi hiyo.

Hii inawaweka watu tayari kuweza kuinua macho na kuishabikia ligi hiyo, hawa walikuwa na dhamira ya dhati ili soka lao litazamwe wapate mikataba ya matangazo wapate fedha. Wakati tunaeleza hayo vuta picha katika nchi yetu (Tanzania) kweli yanafanyika japo sio dunia nzima basi kwa mikoa yote Tanzania?

Wachezaji  wakubwa duniani kupenda kucheza ligi hiyo  kwa msisimko na ushindani uliopo japo unaweza ukasema kama ligi bora kwanini haitoi mchezaji bora jibu lake ni dogo mno kinacho zungunzwa kwanini mashabiki wengi wanapenda ligi ya England. inasemekana kwa Bara hili la Afrika Manchester United ina mashabiki wengi kuliko timu yoyote ile na kwa Tanzania Manchester united ina mashabiki wengi inafuata Arsenal.

UKWELI WA EPL KUITEKA DUNIA KUTAZAMWA
kituo cha supersport mara nyingi kiki onesha mpira wa nchi hiyo haswa mwishoni mwa msimu wana onesha mashabiki wakiwa viwanja mbali mbali duniani wakitazama mpira huo wakiwaa wamevalia jezi za timu zao, hii si kazi rahisi kujiweka katika jambo husika na kuteka dunia.

VIPI TANZANIA INAFANYA HIVI?
 Tunapo liandika jambo  turudi nyumbani kwa sasa tuna nafasi nzuri ya kujitangaza kuna chombo ambacho kina onesha michezo mbalimbali kwanini TFF wasijisogeze kuongea nao ili tuweze kufikisha mbali mpira wetu? Nini kinawashinda au hakuna bajeti hiyo hapa TFF jambo linawahusu.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »