Our Feeds

Monday, 11 April 2016

Unknown

HII NDIO TIMU ILIYOIPISHA LEICESTER CITY LIGI YA MABINGWA ULAYA


Na Amini Nyaungo

Leicester City ni maandishi ambayo kwa sasa kwenye mitandao mbalimbali pamoja na waandishi wanaandika vile watakavyo kwa jinsi mwenendo mzuri na maajabu ya timu hiyo katika ligi kuu  ya England msimu huu.

UNAIJUA HII
Leicester City ndio timu ambayo imeshafuzu kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya mwakani. Manchester United ndio ilikuwa kikwazo baada ya kufungwa jana hata kama akishinda mechi zote na Leicester City afungwe zote hawezi kumfikia Leicester City hivyo mwakani tutaona timu mbali mbali zikifika King Power Studium.

Hesabu ni ndogo tu kwasasa mechi zimesalia 5 zenye jumla ya alama 15 na tayari Leicester City anamzidi Man United kwa pointi 19 kwahyo hakuna namna yoyote ya kuikosa Leicester City kwenye Uefa.

ZAWADI
Mwisho wa msimu huwa kuna kuwa na zawadi kama vile kocha bora wa mwaka,mchezaji bora wa mwaka,wafungaji bora tutaweza kushangaa zawadi hizi ziki miminika Leicester City.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »