Our Feeds

Monday, 11 April 2016

Unknown

HABARI NJEMA KWENYE KIKOSI CHA MAN CITY


Na Albogast Benjamin

Habari njema kwa kocha wa Manchester City baada yakupokea ripoti ya dakatari wa timu hiyo iliyompa nafasi ya kufanya mazoezi leo asubuhi nahodha wake Vincent Kompany na huenda akawepo kwenye kikosi kitakachocheza na PSG kwenye mchezo wa mkondo wa robo fainali ya Uefa kesho.

Wiki iliyopita kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya PSG na Man City, Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany alikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi, ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya mabao mawili. 


Wachezaji wengine walio majeruhi kwenye kikosi hicho ni David Silva,Nicolas Otamendi na Raheem Sterling lakini wanategemewa kurudi kundini mapema kutokana na maendeleo yao kuonyesha nafuu.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »