Na Albogast Benjamin
"Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni" Ni msemo tu wa wahenga na mara nyingi hutokea katika matukio adimu. Tena ikitokea mdogo kamtia adabu mkubwa hapana shaka msemo huu unakuwa umekaa mahala pake.
January 4,2015 kwenye dimba la Anoeta nyumbani kwa Real Sociedad inayoshiriki ligi ya La liga nchini Hispania ulikuwa ni usiku wa aina yake uliowavutia hata wale mashabiki wa Manchester United ambao walikuwa wametoka kufurahia kufukuzwa kwa David Moyes. Real Sociedad chini ya Moyes iliichapa Barcelona bao moja pasipo majibu na jina la Moyes likarejea midomoni mwa watu kwa kishindo.
Usiku wa April 9,2016 Real Sociedad wameonyesha hawakubahatisha etii kwasasabu mechi ya 2015 Messi hakuwepo. Barcelona ikiwa chini ya Messi, Neymar,Iniesta imekubali kichapo cha bao moja bila majibu kutoka kwa timu hiyo yenye makao yake kwenye dimba la Anoeta katikati ya mji wa San Sebastian.
Matokeo hayo yameifanya Barcelona ipoteze alama 6 katika michezo yake miwili ya mwisho baada ya kufungwa 2 - 1 na Real Madrid wakiwa nyumbani. Hivyo sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 3.