Wakati dunia ya mchezo wa kikapu kwasasa ikimtazama Stephen Curry kama "Record Breaker" akitoa rekodi za wakongwe kama Lebron James na Kobe Bryant na kuweka za kwake, upande wa pili dunia ya soka inawatazama watu wawili ambao ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kama "Record Breaker"
Hispania Kwenye La Liga kuna watu wana vunja Rekodi kila kukicha yaani kama wanataka sifa vile Messi na Ronaldo lakini hii imemdondokea Cristisno Ronaldo yeye huwa anaweka na anavunja zake mwenyewe pale Real Madrid.
Bao moja alilofunga kwenye mchezo wa jana dhidi ya Eibar Cristiano Ronaldo aliweka record ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 na zaidi katika misimu 6 mfululizo.
Pamoja na hiyo bado ameweka rekodi kufunga magoli 147 kwa mechi zilizo chezwa Santiago Bernabeu, ambapo aliekuwa anaongoza kwa ufungaji ni De Stefano 145, msimu huu pia kawa mfungaji Bora wa muda wote Real Madrid kwa magoli zaidi ya yale ya Raul 223.