
KIPORO CHA WANA LAMBALAMBA KIMECHACHA
Na Amali Nyaungo
Ama kweli Adui yako usimpige wala usimlipize bali kitu kizuri mshitakie mungu na Waswahili wanasema "Adui muombee Njaa" hii itamfanya ajifunze,Timu ya Simba lazima itakuwa inaomba dua Yanga na Azam viporo vyake vichache na hii wamefanikiwa kwa upande mmoja wa Azam kwani viporo vyake viwili vyote vimechacha.
Leo kulikuwa na michezo miwili ya Ligi kuu ya Tanzania Bara kule Chamanzi Azam wamewakaribisha Ndanda Fc wana kuchele kutoka pale Nangwanda Sijaona, mchezo huu umeenda sare Shufwa ya magoli 2-2 ,magoli ya Azam yalipatikana dakika ya 16 Kupitia zao la Simba Ramadhan Singano "Messi" na la pili lili patikana kupitia Didier Kavumbagu dakika ya 42 wakati ya Ndanda yalipatikana kupitia Atupele dakika ya 42 na A.Morris dakika ya 53 na hadi mwisho Azam 2 Ndanda 2
Wakati huo huo Jahazi la Coast Union linazidi kuzama mara baada ya kukubali kipigo kingine kutoka kwa Maji Maji ya Songea wana Lizombe, Danny Mrwanda alianza kupeleka msiba huo dakika ya 8 wakati matanga yameinuliwa na Lucas dakika ya 48 mwisho wa mchezo huo Maji Maji 2 Coast Union 0
Je, yaliyo mkuta Jose Mourinho au Benitez yatamkuta Stewart Hall?