Our Feeds

Wednesday, 6 April 2016

Unknown

HAYA YOTE YANAWEZEKANA KAMA MOURINHO ATATUA MAN UNITED


Na Amini Nyaungo

Umahiri wake ndio umampa namba pale Old Trafford hilo halina ubishi kiwango cha pesa alicho nunuliwa cha £36m kutoka Monaco kuja Manchester United tena kwa gharama ya kuvunja rekodi kwa vijana wenye umri mdogo kununuliwa kwa bei hiyo, je unahamu ya kumjua nani? subiri kwanza vuta punzi huyo ni Antony Martial fundi mwingine wa France anaefananishwa na Thierry Henry.

KWANINI MARTIAL HAMUHOFII MOURINHO?

 Antony Martial amekataa maswali anayo ulizwa kuwa ujio wa Mourinho huenda ndio ikawa mwisho wake kijana huyo amewajibu waandishi nchini England kuwa ujio wa Jose haumpunguzii wala haumfanyi kiwango kishuke anacho kifanya kufikiria kazi yake na kocha aliepo sasa kama akija Mourinho safi na watafanya kazi ila kwa sasa kazi ndio anayo ifikiria.


UNADHANI KWANINI ANAULIZWA HIVI

Jose Mourinho ni miongoni mwa makocha wenye kuwa na misimamo yao migumu nani alidhani kama Juan Mata angeondolewa Chelsea? nani alidhani Didier Drogba atarudi kucheza Chelsea? hiyo ni mifano midogo nani alidhani licha ya uzee kuwa John Terry ataweza kumuweka benchi? huyu ndio Jose Mourinho,nikocha anae taka mafanikio ya haraka kisha anasepa hata hapo Manchester United akifika hana muda ataondoka na atawaondoa wachezaji ambao wewe huamini  Jibu lake ni hili inasemekana Martial sio chaguo lake na ndio maana maswali yanaanza mapema.

MAISHA YA WACHEZAJI HAWA YAWEZA KUWA NDIO MWISHO OLD TRAFFORD

Juan Mata,Michael Carrick,Marcos Rojo,Antonio Valencia na Phil Jonas orodha ni ndefu lakini hawa wanaweza kupata mlango wa kutokea kama ataifundisha  Manchester United msimu ujao na hayo ndio maisha usifikirie kuwa kila siku utakuwa mahali hapo hapo .

KWANINI NIMEMUACHA WAYNE ROONEY?

Wapenzi wengi wa Manchester United wamechoshwa na Wayne Rooney lakini Mourinho ni kipenzi kikubwa cha nyota huyu kuna wakati alimtaka sana pale Chelsea huyu ndio Jose Mourinho (JM) wao wanmwita “Special moja”

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »