Our Feeds

Tuesday, 5 April 2016

Unknown

MISRI UNDER17 WALALA MARA MBILI MBELE YA SERENGETI BOYS



Na Albogast Benjamin

Mwaka wa furaha mara nyingi huwa wa furaha hii imemtokea Bakari Shime amefanikiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki kupitia timu ya taifa ya watoto chini ya miaka 17 Serengeti Boys na kuweza kupata ushindi mechi zote.

Ameachana na Jkt Mgambo kiroho safi nakujiunga na Serengeti Boys na Nyota huonekana kuchanua mara baada ya kuichapa tena mchezo wa maruduano timu ya watoto wa Misri chini ya miaka 17 magoli 3-2

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Ibrahim Abdallah magoli 2 na moja lilikandamizwa na Boko Selemani wakati ya Misri yalifungwa na Ahmed Saad na Dia Wahed. Stars itaanza kampeni mwezi wa 6 dhidi ya Madagascar.

Je matokeo  ya mechi za kirafiki yataweza kutokea kwenye mashindano? Mtembezisports inaitakia timu hiyo ya Taifa mafanikio.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »