Na Albogast Benjamin
Louis van Gaal amepewa uhakika atakuwa Old Trafford msimu ujao kwa mujibu wa gazeti la Uholanzi De Telegraaf.
Kocha huyo mwenye miaka 64 alisaini mkataba wa miaka 3 mnamo mwaka 2014 lakini amekuwa chini ya shinikizo baada ya kuwa na msimu wa kukatisha tamaa.
Jose Mourinho na Ryan Giggs wote wamekuwa wanaohusishwa na kazi kama kibarua cha Mholanzi huyo kingeota nyasi, kuna uvumi uliokuwa unaendelea kuwa huenda kocha Mourinho aliyefukuzwa ndani ya Chelsea akachukua nafasi ya Van Gaal.
De Telegraaf limetaarifu kwamba Van Gaal ameambiwa ataongezewa kiasi cha Euro 80 ili kuweza kufanya usajili wa wachezaji anaowahitaji ikiwemo jitihada za kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka Everton.