Na Albogast Benjamin
Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekataa ombi la kumtaka awe meneja wa timu ya taifa ya Syria.
Meneja wa kocha huyo Jorge Mendes ametuma barua pepe kwa shirika la habari la Associated Press, amesema Mourinho aliambia Shirikisho la Soka la Syria kwamba “ameshukuru sana kupokea mwaliko, lakini hawezi akaukubali kwa sasa”.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 53 alifutwa kazi na Chelsea kwa mara ya pili Desemba. Mourinho, ambaye amewahi kuwa meneja Porto, Real Madrid na Inter Milan, amehusishwa na kuhamia Manchester United.
Syria kwasasa inakamata nafasi ya 123 kwenye orodha ya viwango vya soka kwa nchi wanachama wa Fifa.