Our Feeds

Monday, 11 April 2016

Unknown

SIMBA NA COSTAL KUISAKA NUSU FAINALI YA FA LEO


Na Jacob Gamaly

TIMU ya Simba leo inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Coastal Union Robo Fainali ya Kombe la FA. Mchezo wa leo licha ya Coastal Union kuonekana haifanyi vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema Coastal Union sio timu ya kuidharau na lolote linaweza kutokea.

Mshindi wa mchezo wa leo ataungana na timu za Yanga, Azam na Mwadui FC, ambazo tayari zimetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA.  Mayanja alisema kikosi chake kimefanya maandalizi ya muda mrefu na kina imani ya kufanya vizuri.

“Tumejipanga kwa mchezo huo na tuna imani mambo yataenda vizuri, lakini sio kwamba tunajiamini asilimia kubwa, kwani Coastal sio timu ya kuidharau kwa sababu haifanyi vizuri, kwani lolote linaweza kutokea,” alisema.
Mayanja alisema wachezaji wake wanaendelea vizuri na wale waliokuwa wamechelewa Hamisi Kiiza na Juuko Murshid wameungana na wenzao tayari kwa mchezo huo.


Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »