Na Amin Nyaungo
Samir Nasri airudisha Manchester City kugombania nafasi tatu za juu mara baada ya kufunga goli la ushindi, ambapo City ili ichapa Westbromwich Albion 2-1
Nasri ni kipaji kinacho sumbuliwa na majeraha mara kwa mara, alikaa nje ya uwanja karibuni nusu msimu wote jana ameonesha thamani yale ndani ya Jiji la Machester hivyo kuwa nyuma ya Arsenal kwa alama 2 Arsenal ina 59 wakati City alama 57.
AMETOKA WAPI?
Marseille ndio timu yake,kutokea 2004 hadi 2008 amecheza michezo 121 na kufunga goli 11 baada ya hapo Arsenal ikamuona ndipo 2008-2011 alipo isaliti timu hiyo na kufanya mashabiki wa arsenal kila aingiapo Emirate anazomewa amecheza michezo 86 amefunga magoli 18 wakati Manchester City tangu 2011 amecheza michezo 123 na kufunga 18 hali kadhalika amestaafu soka la kimataifa timu yake ya France akiwa amecheza michezo 41 na kufunga magoli 5.