Sir Alex Furgason "Leicester City itachukua ubingwa kabla ya mechi Tatu" ni kauli ya kocha mkongwe aliyetunukiwa cheo cha "Sir" baada ya kuifundisha kwa mafanikio makubwa timu ya Manchester United na huenda neno lake hili likawa sheria kwa mwenendo wa ligi ulivyo hivi sasa.
Daraja limevunjwa tena Gylfi Sugurdsson amepeleka kilio Darajani mara baada ya kuisaidia Swansea City kupata ushindi wa goli 1 kwa 0 japo mechi hiyo ilichezwa Libety Studium.
Kiwango kibovu kilichooneshwa na Chelsea ndicho kiliwanyima ushindi endapo Swansea wangekuwa makini wangeweza kufunga zaidi ya goli moja.
MSIMAMO
Chelsea iko nafasi ya 10 ikiwa na Alama 44 nyuma ya Liverpool wakati Leicester City anazidi kupaa angani akifuatiwa na Tottenham Spurs.