Na Amini Nyaungo
Hakuna marefu yasiyo na ncha,Usiye mpenda kaja tunaweza kutumia misemo mingi kwa habari hii ya Kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure baada ya wakala wake Dimitri Seluk kutangaza kuwa ataondoka msimu huu kupitia Sky Sports.
Yaya Toure moja ya viungo hodari ulimwenguni huenda angekuwa amezaliwa ulaya angepata heshima anayo ipata Sergio Busquets au Steven Gerrard kwa kiwango alichonacho mchezaji huyu nyota mara Nne mfululizo wa Afrika. kiungo huyo ilibaki kidogo Wenger amchukue maana aliwahi kufanya majaribio pale Highbury kipindi hiko akiwa kinda.
KWANINI AONDOKE MANCHESTER CITY?
Toure alishawahi kucheza Barcelona kwa mafanikio makubwa haswa nafasi yake ya kiungo ya juu na ya chini. Pep Guardiola alimuondoka Barcelona akiwa na utamu wake kama mua na sasa kocha huyo anarudi na kuja kuifundisha Manchester city, Pengine kutokana na mfumo wa kocha huyo hauendani nae ila ukweli dunia inajua shughuli ya Yaya Toure, na hiki ndicho kilicho sababisha wamiliki wa timu hiyo wachelewe kumpa mkataba hadi kufikia Wakala wake kupitia kituo cha Sky Sports kuwa kiungo huyo ataondoka.
VILABU VIPI VINAMTAKA?
Walio zoea kuchukua wazee ndio wakati wao PSG,Inter Millan na Ac Millan lakini Intern milan anaonekana kuweza kuipata sahihi yake ili ajiunge huko.
Nenda Toure kwa hakika utaacha Athari kubwa England kwa kikubwa ulichofanya,najua John Champion au Jim Beglin watakukumbuka wakati wanatangaza mpira.