
Mkondo wa kwanza Robo fainali ulifanyika usiku wa kuamkia leo ambapo Real Madrid akiwa na BBC yake amekubali kulambishwa oili ya watengeneza magari wa aina ya Wolfsburg magoli 2-0, kwa matokeoa hayo inatakiwa wapate Magoli 3-0 ili wapite hatua inayo fuata ya Nusu fainali vinginevyo watatupwa nje ya michuano hiyo.
Wakati huo huo Manchester City na PSG wote walishindwa kutambiana mara baada ya kutoa sare shufwa ya magoli 2-2 kila mmoja alitaka kutengeneza rekodi, magoli ya City yalifungwa na Fernandinho na Kevin De Bruyne wakati ya Psg yalifungwa na Ibrahimovic na Rabiot.