Our Feeds

Thursday, 7 April 2016

Unknown

MAAMUZI MAGUMU YA WENGER DHIDI YA JACK WILSHERE


Na Amini Nyaungo

Unaweza kuwa na kipaji kikubwa lakini kitu kinaitwa Majeruhi kinaweza  kukukwamisha na kukupoteza katika ramani ya mchezo huu wa mpira. 

Jack Wilshere ni kiungo wa Arsenal alie jaaliwa kipaji katika mchezo wa mpira Pep Guardiola alishawahi kusema kuwa Wilshare inawezekana hakuzaliwa England kutokana na uwezo wake na kasi, kiungo huyo ameuguza majeraha yake ya  goti msimu wote wa 2015-2006 na sasa amerejea.

Taarifa zinasema kuwa Wenger amemrudisha kikosi B chenye chini ya Miaka 21 ambacho kitacheza ijumaa hii dhidi ya Newcastle United ili aweke sawa kipaji chake na hii ni kampeni ya kuwa sawa kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya.

Wakati huo kiungo mkongwe Tomas Rosicky atacheza mchezo huo wa kesho dhidi ya Newcastle ili nae ajiweke sawa na viungo wengine Aaron Ramsey na Metheu Flamin watajumuishwa katika mchezo wa kikosi cha kwanza utakaochezwa jumamosi dhidi ya Westham.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »