Our Feeds

Tuesday, 5 April 2016

Unknown

REKODI ZA AUBAMEYANG NDANI YA BUNDESLIGA HIZI HAPA

Na Albogast Benjamin
Unaikumbuka vyema siku ya January7 pale Jijini Abuja Nigeria ndani ya ukumbi wa ABUJA CONFERENCE CENTRE, wakati watanzania wanashangilia Samatta kuweka rekodi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wa ndani ndio siku ambayo Yaya Toure alichukia tuzo hizo baada ya kuzifurahia mara nne akiamini anakwenda kuvuka rekodi ya Samuel Eto'o ili achukue mara tano lakini Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang ndiye aliibuka mshindi.
Unazijua rekodi anazoziweka Pierre Kunako Bundesliga?
Mchezaji huyo kutoka Gabon ndiye mchezaji kutoka Afrika aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga msimu mmoja.
Aubameyang alifunga bao dhidi ya Werder Bremen Jumamosi na kufikisha idadi ya mabao 23 aliyofunga msimu huu.
Rekodi ya awali ilikuwa ya mabao 22 na iliwekwa na Cisse Papiss wa Senegal msimu wa 2010/11. Papiss kwa sasa anachezea Newcastle United ya Uingereza.
Msimu huu wa 2015/16 pia, Aubameyang alikuwa ameweka rekodi kwa kufunga bao katika kila mechi mechi nane za kwanza za msimu wa Bundesliga, akiipita rekodi ya awali kwa mechi mbili.
Kwa kuwa alikuwa amefunga mabao mechi mbili za mwisho za msimu wa 2014-15, alivunja rekodi nyingine ya kufunga mabao mfululizo katika mechi 10 za Bundesliga. Mtu pekee aliyekuwa ameifikia ni Klaus Allofs miaka 30 iliyopita.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »