Our Feeds

Monday, 4 April 2016

Unknown

UHONDO WA UEFA NA REKODI ZAKE HUU HAPA TENA



Na Amini Nyaungo

Wakati Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizidi kutupa raha kufuta sikukuu ya Muungano na pesa kusaidia mambo ya kijamii, Karibu mwana michezo mwenzangu,karibu Uefa Champions League karibu tena tumekumisi hatua inayofuata sasa ni Nane bora ama Robo fainali ambapo vidume vinane vimeingia katika hatua hiyo. Kuna timu zimeingia kwa mara ya kwanza na wengine wataenda kuandika historia maana hawajawahi kuingia Robo na nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Duniani.

TIMU GANI ZITAWEKA HISTORIA?

Manchester City dhidi ya Paris saint Germain,Uefa kama wameangalia vile kumbe ndio chekecha limecheketua na kuvipata vilabu hivi kukutana hatua ya Robo fainali, Manchester City imeingia kwa mara ya kwanza Robo fainali na kama itafanikiwa ikiingia Robo fainali itakuwa imeandika historia nyingine klabu hiyo kwani haikuwahi kuingia hatua hiyo, wakati hayo yakiendelea PSG nao kama wakiingia Nusu fainali itakuwa mara ya kwanza kuingia hatua hiyo katika historia ya timu hiyo,hivyo yoyote anaweza kuandika historia na nafasi wanayo.

RAHA IKO WAPI?
Raha itakuwa pale Barcelona anapo kutana na Atletico Madrid kupigania nafasi ya kucheza nusu fainali kesho majira ya saa 21:45 je ataweza kuepuka vichapo mfululizo kutoka kwa timu zinazo toka Mji wa Madrid? jibu lipo kesho au waulize watu wa mikeka wanavyo fikiria.

JUMANNE
BARCELONA VS ATLETICO MADRID
BAYERN MUNICH VS BENFICA

JUMATANO
PSG  VS MANCHESTER CITY
WOLVSBURG VS REAL MADRID.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »