Na Amini Nyaungo
Wakati tunashuhudia Kadi nyekundu inatoka kwa Fernando Torres nusu fainali ya Uefa Champions League dhidi ya Barcelona na mchezaji huyo kukiri kuwa kosa lake na litarekebishwa marudiano.
Leo ni siku muhimu sana kwa Manchester City na Paris St Germain kama mtembezisports ilivyo ainisha siku za nyuma kuwa timu hizi hazikuwahi kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo hivyo yoyote atakae pita ataweka historia leo ni mkondo wa kwanza (First leg).
MAKOCHA WA TIMU
Manuel Pellegrini huyu ni raia wa Chile alishawahi kuifundisha Real Madrid msimu mmoja 2009-2010 ni kocha ambae hana maneno mengi yeye anaondoka msimu huu atataka kuweka historia ya Manchester City na kuiweka vizuri Cv yake hata aendapo iwe rahisi kupata ajira, Laulent Branc nayeye aliwahi kuifundisha timu ya Taifa France 2010-2012 naye inasemekana ataondoka ataweka historia endapo ataingia nusu fainali
MTAZAMO
Timu zote zina wachezaji wazuri upande wa kati kuna Fernando na Fernandinho ikitiwa chachandu na Yaya Toure wakati yupo kiungo muongo muongo David Silva mbele yupo kubwa la Maadui Sergio Aguero, kwa upande wa Psg wapo kamili Kuna Verrati,Matuidi,Pastore pia lulu iliyo achwa na Van Gaal Di Maria pia iko kiboko yao Ibrahimovich "Ibracadabra" utakosaje kuangalia mechi. kutakuwa na mchezo mwingine wa hatua hiyo REeal Madrid watacheza na Wolfsburg muda huo huo.
Kimsingi ni mechi nzuri sana itakayo chezwa usiku wa leo saa Tatu na dakika Arobaini na tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki (21:45) huu muda wako wewe kijana ambae umezaliwa katika kizazi cha Messi na Ronaldo, Ronaldinho na kaka, Ronado de Lima na Zidane,kutazama na kupata cha kusimulia kizazi kijacho.