Our Feeds

Wednesday, 13 April 2016

Unknown

YANGA NA AZAM KUUSAKA UBINGWA LEO


Na Jacob Gamaly

YANGA na Azam leo zinatarajiwa kushuka kwenye viwanja tofauti katika mechi za viporo Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo kama zitashinda zitapunguza pengo la pointi na vinara wa ligi hiyo, Simba.

Simba inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 24, wakati Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 53, ikiwa na michezo 22, huku Azam ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 52 baada ya kucheza mechi 23.

Mabingwa watetezi Yanga watakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikabili Mwadui ya Shinyanga, huku Azam FC ikiwa Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar iliyopo nafasi ya nne ikiwa na pointi 34.

Yanga itaingia uwanjani baada ya Jumamosi kulazimishwa sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo zitarudiana Jumatano wiki ijayo nchini Misri.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »