Na Amini Nyaungo
Mchezo wa mpira wa miguu una vitu vingi vidogo vidogo lakini vina thamani kubwa katika mpira. Mashuti mara nyingi huwa yanaleta Magoli Roberto Carlos alikuwa Hodari wa kupiga Mashuti aliwahi kupiga faulo umbali mrefu ikaenda pembeni na hatimae ikaingia Golini pia Paul Scholes mwingereza aliekuwa na Roho ya paka kwa Mashuti.
Manchester United msimu huu haipo sawa kwani ni ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa upigaji wa mashuti na hiki ndio chanzo cha kukosa hata kuzipata nafasi nne Bora katika idadi hiyo ya upigaji mashuti Tottenham Spurs ndio inaongoza kwa kupiga mashuti.
IDADI KAMILI HII HAPA
1.Tottenham Spurs 413
2.Manchester city 381
3.Arsenal 350
4.Westham United 338
5.Southampton 337
6.Leicester city 331
7.Liverpool 330
8.Chelsea 318
9.Crystal Palace 301
10.Everton 292
11.Bournemouth 281
12.Stoke city 279
13.Swansea City 276
14.Sunderland 271
15.Norwich 271
16.Watford 254
17.Aston villa 248
18.Newcastle United 247
19.Manchster United 237
20.Westbromwich Albion 222
Mpira ni starehe ya kipekee ambayo ina mashabiki wengi Duniani kote Manchester United wajiulize Ferguson kaondoka na Manchester yake?