Na Amini Nyaungo
Wimbi la kutimuliwa kwa makocha linaendelea sasa upande wa makocha wa Serie A kocha wa Ac Milan Sanisa Mihajlovic atimuliwa baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Mihajlovic ametimuliwa kwa kukosa mwenendo mzuri wa timu hiyo baada ya kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Juventus ambayo iko nafasi ya kwanza.
Juventus ina Alama 76 na inayomfuata Napoli ina Alama 70 huku Ac Milan ina Alama 49
NANI KATEULIWA?
Cristian Brocch ndie atakaeshika wadhifa huo kwa muda hadi msimu ukiisha ili waajili kocha mwingine wa kudumu Brocch sasa atakuwa kocha wa 5 kuifundisha Ac Milan kwa kipindi cha Miaka 3 iliyopita.