Unapotaja kati ya mabondia wakali duniani huwezi acha kumtaja Muhammad Ali, Mike Iron Tyson,Frank Bruno na Evender Holyfield wapo wengi wababe wa Masumbwi hata kwetu lazima utaje Rashidi Matumla,Maneno Osward na Francis Cheka.
UNAMJUA DEONTAY LESHUN WILDER?
Huyu ni mbabe mwingine ambae kwa wafuatiliaji wa Ngumi wana mjua haswa kwa Rekodi zake za kuvutia katika kuwachapa wapinzani, Deontay ni Raia wa America ana urefu wa futi sita na amezaliwa 22,10,1985 Tuscaloosa Alabama nchini Marekani.
REKODI
Amepigana mara 36 mashindano ya kimataifa ambayo yana tambuliwa na chama cha Masumbwi Duniani na kushinda yote 36, akipiga Knock Out (KO) 35 na moja alishinda kwa Alama (Point).
Katika hayo 35 aliyo piga 'KO',18 amepiga 'KO' Round ya kwanza. huo mmoja alio shinda kwa Alama ulikuwa na Bondia Canada mwenye asili ya Haiti Bermane Stiverne kwa Round 12 .
MAISHA BINAFSI
Ana watoto 4 wakike Naiyeya na Ava wakiume Dereon na Deontay Jr. alimuoa mpenzi wake Jesca Scales Wilder mwaka 2009.
UTATA
MAY 4, 2013 alikamatwa na polisi baada ya kuwa na leseni bandia baadae aliomba radhi.
PAMBANO LINALOFUATA
21/05/2016 atapanda tena ulingoni kwa ajili ya kutetea ubingwa wake wa WBC dhidi ya Alexander Povetkin ndani ya Jiji ka Moscow ambapo huyu anae kutana nae sio mnyonge kapigana mapambano 30 na 22 amepiga Knock Out.