Our Feeds

Tuesday, 12 April 2016

Unknown

HUYU NDIO KOCHA BORA LIGI YA KENYA


Na Albogast Benjamin

Kocha Mkuu wa AFC Leopards  Ivan Minnaert ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Machi kwenye ligi kuu ya soka Kenya. Tuzo hiyo inayoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari Kenya (SJKA).

Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa wa pili kutwaa tuzo hyo baada ya kocha wa Mathare United Francis Kimanzi kuchukua mwezi Februari.

"Nimepatwa na msisimko kupokea hii tuzo ya kifahari na lazima niseme imetokana na kazi nzuri ya benchi zima la ufundi na wachezaji. Nina hakika SJAK watarejea hapa mara nyingi zaidi kwa sababu sisi tuna  kwenda kufanya vizuri msimu huu" Minnaert aliuambia mtandao wa supersport.com.

Minnaert alijiunga Leopards katikati ya Februari na amekuwa na rekodi nzuri Machi hadi kuongoza msimamo wa ligi ya Kenya maarufu kama SportPesa Premier League. Ameshinda dhidi ya  GOtv Shield mabingwa Bandari, wapinzani wao Gor Mahia na Kakamega Homeboyz alipoteza pointi dhidi ya Chemelil Sugar.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »