Our Feeds

Friday, 8 April 2016

Unknown

AC MILAN KUMRUDISHA LIVERPOOL BALOTELLI


Na Amini Nyaungo

Super Mario Balotelli ni moja ya wachezaji walio na kipaji cha hali ya juu anaweza kufanya chochote uwanjani, Haswa kumbukumbu ya ya uwezo wake wa kupiga penati bila kukosa. Lakini ujeuri na utukutu wake ndio una mnyima ulaji katika timu nyingi.

SAFARI YAKE YA MPIRA

Watu walianza kumfahamu na kumfuatilia pale alipo kutana na Robert Mancin Inter Milan nyota yake ikachanua na ndipo akaelekea Manchester City huko akakichafua sana na alikuwa lulu na moja ya mechi aliyoweka rekodi ni ile ya kuifunga Manchester United kisha akaonesha maandishi yakisomeka "Why Always Me?" kisha akaenda Liverpool ambapo yupo hadi sasa lakini katolewa kwa mkopo Ac Milan.

NINI KINA MSHINDA?

Balotelli ni mtukutu sana hiki ndicho haswa kinacho mnyima kukaa na makocha wengi, hivi karibuni ametolewa kwa mkopo Ac Milan  amecheza michezo 17 na kufunga Magoli 3 na anataka kurudi Epl. ingawaje amebadilika nidhamu kwa maelezo ya wachezaji wenzake Ac Milan kinacho mfanya ashindwe ni nidhamu hakuna kingine.

ANARUDI LIVERPOOL

Mtendaji mkuu wa Ac Milan Adriano Gallian amesema kuwa mchezaji huyo hakufika malengo waliyo yaweka endapo angefikia malengo  huenda wange msajili moja kwa moja. Je Jurgen Klopp ata weza kuvumilia utukutu wake? lakini vipi kwa maelezo tuliyowahi kusikia kupitia sky sports kuwa wachezaji wa Ac milan wanasema kabadilika ni kweli.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »