Our Feeds

Friday, 8 April 2016

Unknown

PAMBANO LA TYSON NA WLADMIR KUPIGWA JIJINI MANCHESTER TAREHE HII



Na Albogast Benjamin 

Baada ya pambano la Novemba mwaka jana kati ya Fury na Klistschko lililompa ushindi Tyson Fury sasa tarehe ya pambano la marudio imetangazwa na Peter Fury mwalimu na mjomba wa Tyson Fury.
  
Pambano hilo  la marudio kati ya Tyson Fury na Wladmir Klitschko litaandaliwa mjini Manchester mnamo mwezi Julai tarehe 9 kulingana na mkufunzi wa bondia huyo wa Uingereza.


Peter Fury ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter siku ya Ijumaa na tangazo jingine linatarajiwa baadaye.

Fury ambaye ni mzaliwa wa mjini Manchester na ambaye ana umri wa miaka 27,alimshinda raia wa Ukraine Klitschko kwa pointi mjini Dusseldorf mwezi Novemba ili kushinda mikanda mitatu ya WBA,IBF na WBO.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Fury ni Muingereza wa tano kushinda mataji hayo ya uzani mzito zaidi duniani.

Hatahivyo Fury alipokonywa ukanda wa IBF wiki mbili baada ya ushindi huo na marudiano na Klitschko yanamaanisha kwamba hatokabiliana na bingwa wa uzani huo Vyacheslav Glazkov.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »