Our Feeds

Monday, 4 April 2016

Unknown

AJALI YAMNYIMA UBINGWA LEWIS HAMILTON WA BAHRAIN GRAND PRIX

Na Albogast Benjamin
Dereva wa magari yaendayo kasi maarufu kama Formula one Nico Rosberg wa timu ya Mercedes ametwaa ubingwa wa michuano ya Bahrain Grand Prix.
Rosberg alipata ushindi huku akimzidi dereva mwenza wa timu yake Mwingereza Lewis Hamilton ambae gari lake liligongana na dereva wa ferarri katika raundi ya kwanza.
Dereva wa timu ya Ferrari Kimi Raikkonen alishika nafasi ya pili katika michuano hiyo.Huku Lewis Hamilton akiambulia nafasi ya tatu.
Ushindi wa dereva huyu ni watano mfululizo na kumpa nafasi ya kuongoza kwa alama 17 mbele ya Lewis Hamilton.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »