Our Feeds

Monday, 4 April 2016

Unknown

KIBONZO CHA WIKIENDI SIMBA DHIDI YA NIDHAMU FC


Na Albogast Benjamin

Jana funga wiki ya hatari ilifanyika pale uwanja wa Chuo cha polisi asubuhi tu ulipopigwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba SC na Nidhamu FC. Simba wakiitumia mechi hiyo kama sehemu ya mazoezi ya kujiweka fiti na mwendelezo wa ligi kuu baada ya wikiendi hii kutokuwa na mchezo.

Simba ikiwa na mchanganyiko wa kikosi cha kwanza na wengine kutoka kikosi B ilifanya mauaji ambayo nadhani kama ingekuwa kwenye ligi au mashindano rasmi uchunguzi huenda ungechukua nafasi yake ili kujiridhisha kama hakuna namna yoyote ya kupanga matokeo.

Dany Lyanga aliondoka na mpira wake baada ya kufunga mabao matatu yaani "Hatrick", Awadh Juma yeye akapiga mawili wakati Said Hamis Ndemla,Hassan Isihaka, Ibrahim Ajib, Peter Mwalyanzi, Musa Mgosi na Moses kutoka Simba B walifunga bao moja kila mmoja hivyo kufanya matokeo kuwa mabao 11 kwa 1 la Nidhamu FC. 

Ama kweli hiki ni kibonzo cha wiki.. mtembezisports inakutakia wiki njema.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »