Na Amini Nyaungo
Antonio Conte amewasili nchini England kwa ajili ya hatua za awali za kusaini mkataba na Chelsea kuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo ambayo inanolewa na Guuss Hiddink hadi mwishoni mwa msimu.
Kocha huyo ameonekana nchini humo leo na gazeti la Gazzate delle Sports limeripoti kuwa kocha huyo atapewa mkataba wa kuifundisha timu hiyo miaka 3 wenye thamani ya £15m.
Conte ni kocha wa timu ya taifa ya Italy na kinacho subiriwa yaishe mashindano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro yatakayofanyika June mwaka huu ndipo achukue hatamu klabuni hapo, Kocha huyu wa zamani wa Juventus hapo awali alikataa kuhusishwa na Chelsea lakini sasa mambo wazi kabisa.
Timu ya Chelsea ilikuwa chini ya Mourinho msimu uliopita ambapo walichukua kombe la Epl lakini mambo hayakuwa vizuri msimu huu kutokana na timu kutofanya vizuri na kupelekea kutimuliwa kwa kocha huyo mwenye umaarufu wa kubwabwaja pindi anapokuwa anashinda.