Na Amini Nyaungo
Arsene Wenger ni mmoja ya makocha mahiri kabisa Duniani, Kocha huyu ana sifa kubwa ya kuweza kujua vipaji vya wachezaji Duniani, hawa ni moja ya wachezaji aliowahi kuwaota wakiwa makinda na kushawishi kuwa nunua ila akashindwa kuwachukua kutokana na ubahiri wake.
1.Cristiano Ronaldo huyu ilikuwa tayari kila kitu na ilitakiwa safari tu apande ndege aje Highbury lakini ujanja wa Ferguson na kocha msaidizi wa kipindi hiko alikuwa Mreno aka mshawishi Ronaldo kutua Old Trafford lakini sababu nyingine imeelezwa pesa zili mfanya abadili maamuzi.
2.Gareth Bale kijana huyu kutoka Wales zamani alikuwa anacheza beki namba 3 wakati anatua England Wenger ndio kamshawishi na akakubali lakini dakika za mwisho anatua kwa Majirani Tottenham Spurs na kocha Harry Rednapp ana mbadilisha na kumchezesha pembeni.
3.Juan Mata huyu Fundi mwingine ana degree ya Uandishi wa habari wakati anatoka Hispania wenger ilikuwa lengo lake aje Emirate tatizo pesa akashindwa kulipa akaenda Chelsea
4.Yaya Toure Kiungo mahiri Duniani wakati anatoka Ivory Coast wenger alimleta kufanya majaribio kilicho mfanya ashindwe kuendelea hadi leo hakifahamiki hatimae anatua Barcelona
5.Edin Hazard huyu waziwazi Wenger ameshindwa kutoa fungu ili amchukue winga huyu.
6.Zlatan Ibrahimovic Ukiona Kadabra anatia nyodo katika Tetesi za kutua Arsenal kuwa hataki kuja hapo alikuja kujaribu majaribio lakini wenger katika malipo kama kawaida yake akashindwa
7.Lionel Messi unaweza usiamini kwa hiki kinacho elezwa ila wenger ilishawahi kumfukuzia nyota huyu wa wakati wote Duniani.