Our Feeds

Friday, 8 April 2016

Unknown

KLOPP AWAZUIA VIJANA WAKE WA ZAMANI


Na Amini Nyaungo

Naam,Filimbi ya mwamuzi maarufu kutoka nchini Hispania Carlos Velosa pale iduna park akiashiria mpira kumalizika Borrusia Dortmund 1 Liverpool 1, ni mchezo uliojaa ufundi wa kila aina na kasi ya aina yake  huku Jurgen Klopp akipata mapokezi mazuri baada ya kuondoka msimu uliopita.

Liverpool walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wa Ubeligiji mwenye asili ya Kenya Devok Origi Dakika ya 36 bao hilo lilienda hadi kipindi cha kwanza kuisha. Dakika ya 48 kipindi cha pili beki Mats Hummels aliiandikia Dortmund bao la kusawazisha kuanzia hapo umiliki wa mpira ukawa kwa Dortmund.

TATHIMINI YA MCHEZO

Mashuti yaliyopigwa Golini Borrusia Dortmund 7 na Liverpool 6, wakati mashuti yasiyo kuwa na malengo Liverpool 3 na wenyeji 3, Mipira ya kuotea Liverpool 4 na Dortmund 1, wakati kona Borrusia 5 Liverpool 1, madhambi wenyeji 13 wageni 14 huku wote walibadilisha wachezaji mara 3 kila mmoja na umiliki wa mpira Dortmund 59% na Liverpool 41.

Matokeo haya yaweza kuwa faida kwa Liverpool kwakuwa wamepata Goli ugenini lakini katika mpira lolote linaweza kutokea. Tusubiri mechi ya marudiano Juma lijalo.

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE
Athletic Club 1 Sevilla 2
Braga 1 Shakhtar Donetsk 2
Villareal 2 Sparta Brague 1 

Je Liverpool ya Klopp itaweza kurudisha Heshima iliyo potea? tusubiri hadi mwisho wa msimu.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »